Amana ya Mda Maalum
- Service Type: Deposits
- Date Created: 1 year ago
Amana ya Mda Maalum
Mwanachama akitaka kufunga akaunti hii, atapoteza sifa za kupata faida zilizozalishwa katika mwaka husika
Utaratibu wa akaunti hii, utakuwa kama ifuatavyo,
- Mhusika atajaza fomu ya mkataba ya kufungua akaunti hiyo.
- Akaunti hii haitozwi gharama za kufungua akaunti.
- Kiwango cha chini cha kufungua akaunti hii ni Tsh 2,000,000/=
- Mteja haruhusiwi kuchukua fedha kutoka akaunti hii hadi hapo mda wa mkataba utakapoisha
- Riba zitakazolipwa kwenye akaunti ya amana maalum zitakuwa kama ifuatavyo.
Miezi 3 |
Miezi 6 |
Miezi 9 |
Miezi 12 |
5% p.a |
7% p.a |
8% p.a |
11% p.a |
- Kiasi kitakachoanza kulipwa riba ni kuanzia Tshs. 2,000,000
- Kama mwanachama ameamua kuvunja mkataba kwa kuchukua fedha kutoka akaunti hii kabla ya muda, itamlazimu kukosa faida ambayo angeipata katika kipindi hicho.
- Mwanachama anayetaka kuchukua au kuongeza kiasi na muda katika akaunti ya Amana ya Muda Maalum atahitajika aonyeshe mkataba na stakabadhi iliyotumika wakati wa kuweka au kufungua akaunti.
- Mwanachama aliyepoteza stakabadhi, atawajibika kuleta taarifa ya Polisi inayothibitisha upotevu huo; stakabadhi mpya itatolewa baada ya muda wasiku kumi na nne (14) za kazi na mhusika atawajibika kuchangia shs. 10,000/=.